• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uandikishaji wa wanaridha kwenye mbio za Ngorongoro waanza

    (GMT+08:00) 2020-08-20 19:11:10

    Wanariadha mbalimbali wamejitokeza kwa wingi siku ya kwanza ya kujiandikisha kushiriki Ngorongoro Race 2020, katika Kituo cha Arusha, wakitaka kushiriki mbio hizo zitakazofanyika Septemba 19. Mratibu wa mbio hizo ambazo hufanyika kila mwaka, Meta Petro, amesema wanariadha wengi juzi walijitokeza katika kituo cha usajili kilichopo Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kwa ajili ya kujiandikisha. Mbali na jijini Arusha, kituo kingine cha kuandikisha wanariadha wanaotaka kushiriki mbio hizo kipo Karatu zilipo ofisi za Ngorongoro Race. Alisema ni matarajio yake wanariadha nyota kama Alphonce Simbu, Failuna Abdi, Sara Ramadhani watajiandikisha kushiriki mbio hizo. Mbio za mwaka huu, ambazo awali zilitakiwa kufanyika Aprili na kuahirishwa hadi Agosti Mosi kabla ya kusogezwa mbele tena hadi Septemba 19, zitakuwa za aina yake, ambapo kila mshiriki atakayemaliza mbio, atakabidhiwa medali. Ngorongoro Race 2020 pia zitashirikisha mbio za kilometa 21, 10 na 2.5 kwa watoto wadogo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako