• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uganda:Mauzo ya maua yafufuka,yaongezeka kwa asilimia 30.

  (GMT+08:00) 2020-08-20 20:02:58

  Usafirishaji maua nchini Uganda umefufukakatika kipindi kilichoisha mwezi Juni baada ya kuathirika pakubwa kutokana na janga la Covid-19.

  Mwezi Machi,Chama cha Wasafirishaji Maua cha Uganda kiliripoti kuwa mauzo yameshuka kwa asilimia 90.

  Hata hivyo,kwa mujibu wa Benki Kuu ya Uganda,bidhaa hiyo imekuwa ikipata afueni tangu mwezi Mei na kuandikisha mauzo ya $4.2m (Shs15.5b) katika mwezi huo wa Mei.

  Kulingana na Benki hiyo,mauzo ya maua yaliimarika mwezi Juni na kuandikisha mapato ya $6m (Shs22b), ambayo yanawakilisha ufufukaji wa asilimia 30.

  Wadadidi wanasema utendaji huo umeimarika kutokana na kuongezeka kwa idadi ya ndege za mizigo zinazoingia na kutoka Uganda.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako