• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: Mradi wa kuimarisha viwanda kwa kuongeza tija waokoa Sh.300m

  (GMT+08:00) 2020-08-20 20:03:23

  Serikali ya Tanzania imesema mradi wa kuimarisha viwanda kwa kuongeza tija katika uzalishaji na ubora wa bidhaa zinazozalishwa (KAIZEN), umeokoa Sh. milioni 300 ambazo zingetumika visivyotarajiwa viwandani.

  Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof. Riziki Shemdoe, alipokuwa akizindua Mpango wa Kitaifa wa uongezaji endelevu wa ubora na tija katika sekta ya uzalishaji viwandani kwa mwaka 2020 hadi 2030, uliosimamiwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA).

  Akizindua mpango huo katika maadhimisho ya Siku ya KAIZEN, alisema katika mwaka 2019/20 wizara ilifanya tathmini ya hali ya utekelezaji wa mradi wa KAIZEN, na kubaini kuna ongezeko la ubora na tija kwa bidhaa za viwandani kutokana na usimamizi bora ambao umeokoa kiasi hicho cha fedha.

  Aidha, Prof. Shemdoe alisema Rais John Magufuli ameonyesha wazi kuwa anatumia falsafa ya KAIZEN katika miradi mingi inayotekelezwa kwa fedha za serikali.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako