• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Utalii waathirika Baringo baada ya korongo (flamingo) kutoroka mafuriko

  (GMT+08:00) 2020-08-20 20:03:39

  Utalii katika kaunti ya Baringo nchini Kenya umepata pigo baada ya maelfu ya ndege aina ya korongo au flamingo kuhama kutoka Ziwa Bogoria kutokana mafuriko.

  Mapema mwaka huu,zaidi ya milioni ya ndege hao walihamia Ziwa hilo baada ya kuzaliana katika Ziwa Natron nchini Tanzania.

  Hata hivyo maelfu wamebadili makazi na kuhamia Ziwa Nakuru,ziwa Elemtaita na Lokipi katika kaunti ya Turkana,kutokana na viwango vya juu vya maji ambavyo vimetatiza utafutaji chakula.

  Mwezi Januri mwaka huu ,ndege hao zaidi ya milioni,walihamia Ziwa Bogoria mapema kuliko ilivyotrajiwa.

  Kwa kawaida tukio hilo hufanyika mwezi Mei ambapo Ziwa hilo mwenyeji wa takriban nusu ya idadi ya korongo au flamingo duniani baada ya kuzaliana.

  Ndege hao kwa kawaida huhamia Tanzania mwezi Novemba kwa ajili ya kuzaliana na kurudi Kenya katikati ya mwezi Juni.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako