• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ujenzi wa kituo kipya (Terminal 3 ) katika uwanja wa ndege Zanzibar kukamilika Septemba

    (GMT+08:00) 2020-08-20 20:03:58

    Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar,Mohamed Ramia Abdiwawa amesema uchumi wa Zanzibar utaendelea kukua kupitia sekta ya utalii baada ya kumalizika ujenzi wa uwanja wa ndege.

    Akikagua ujenzi kituo kipya cha abiria cha Terminal 3 unaoendelea katika uwanja wa ndege wa Abeid Karume kisiwani Zanzibar jana,Abdiwawa alisema uwanja huo utatoa fursa zaidi za biashara kwani una uwezo wa kuchukua abiria zaidi ya million moja kwa wakati mmoja.

    Meneja wa ujenzi wa Uwanja huo Yaser De Costa alisema ujenzi unaendelea vizuri na hivi sasa umefika asilimia 86 ,huku ukitarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka huu.

    Kituo hicho kipya kina uwezo wa kuchukua ndege 4 kwa pamoja na kinatarajiwa kufunguliwa Septemba 22 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako