• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Lionel Messi aendelea kuwaweka njia panda Barcelona, asema anaondoka

    (GMT+08:00) 2020-08-21 17:43:07

    Nyota wa Klabu ya Barcelona, Lionel Messi amemwambia kocha wake mpya Ronald Koeman kwamba hana matumaini ya kuendelea kubaki ndani ya klabu hiyo. Messi anaripotiwa kufanya mazungumzo ya ana kwa na na Koeman ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili kuinoa klabu hiyo ambayo imetoka kupoteza mechi kwa aibu ya magoli 8-2 mbele ya Bayern Munich. Inatajwa kuwa Messi ameweka wazi kuwa hana imani na mkuu wa Klabu ya Barcelona Josep Bartomeu, hivyo anatazama maisha yake ya baadaye. Kuna habari kuwa Messi anaweza kuibukia ndani ya Klabu ya Manchester City iliyo chini ya Kocha Mkuu, Pep Guardiola ambaye awali alikuwa anaamini kuwa Messi anapaswa kumalizia maisha yake ya mpira ndani ya Barcelona, hivyo kwa sasa anaweza kuwashawishi mabosi wake wampe dili nyoa huyo mwenye miaka 33. Koeman amesema itakuwa vigumu kumshawishi mchezaji ambaye anahitaji kuondoka ndani ya kikosi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako