• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bayern Munich na PSG kukutana jumapili katika mechi ya fainali Champions League

    (GMT+08:00) 2020-08-21 17:45:46

    Kombe la klabu bingwa Ulaya pia linafika tamati wikiendi hii kwa mechi ya kukata na shoka kati ya PSG ya Ufaransa na Bayern Munich ya Ujerumani. Hatimaye uwekezaji wa muda mrefu na uvumilivu wa Paris Saint German umelipa, kwani baada ya kuwa nje ya nafasi za juu kwenye ligi za Ulaya, sasa imefika hatua ya fainali. Wafaransa wanagombea timu hiyo ipate kombe hilo ambalo limekuwa adimu kwa Ufaransa kwa muda mrefu sana. Mafanikio ya klabu za Ufaransa, ikiwa ni pamoja na Lyon ambayo imetolewa na Bayern Munich katika hatua ya robo fainali, yanafuatilia mafanikio ya timu ya taifa ya Ufaransa ambayo kwa sasa ndio bingwa mtetezi wa kombe la dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako