• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kampuni zatakiwa kutenganisha taka

  (GMT+08:00) 2020-08-21 19:25:01

  Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) imezitaka kampuni za ukusanyaji taka kutenganisha taka za kawaida na za kemikali ili kuzuia madhara kwa jamii.

  Akitoa rai hiyo, ofisa mkuu mkaguzi wa GCLA Emmanuel Lewanga alisema kampuni zinazozoa taka zimekuwa zikichanganya taka hizo na kuna haja ya kuziteketeza ili zisilete madhara kwa jamii inayozunguka eneo zinakoteketezewa.

  Kwa upande wake, mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Jumanne Shauri amesema maofisa wake wataanza harakati za kuwatambua na kuwasajili wafanyabiashara wanaojihusisha na kemikali kwa kushirikiana na Ofisi ya Kanda ya Mashariki.

  Alisema watahakikisha maofisa hao wanashirikiana na mamlaka, katika kuhakikisha wanapata barua za utambulisho au usajili kabla ya kupewa leseni ya biashara.

  Shauri aliendelea kusema kuwa, watashiriki katika kufanya ukaguzi wa kutambua wafanyabiashara ambao walipewa leseni za biashara na wanajihusisha na biashara ya kemikali bila kutambuliwa na mamlaka kwa lengo la kusaidia wasajiliwe ili kulinda afya za wananchi na mazingira kwa sababu kemikali ni hatari zisiposimamiwa kikamilifu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako