• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mamlaka ya kudhibiti sekta ya bidhaa za maziwa Kenya kulinda wakulima

  (GMT+08:00) 2020-08-21 19:25:22

  Mamlaka ya kudhibiti sekta ya maziwa nchini Kenya imewaahakikishia wakulima kuwa mikakati inawekwa kuwalinda kutoka kwa uagizaji wa bidhaa za maziwa kutoka nje wakati huu ambapo Kenya inatafuta ushirikiano wa kibiashara na Marekani. Mamlaka hiyo imesema ni wazi kuwa uagizaji wa bidhaa za maziwa kutoka nje utakuwa tishio kwa sekta hiyo nchini Kenya hata hivyo haikueleza zaidi kuhusu hatua watakazochukua kuwalinda wakulima hao. Mamlaka hiyo imesisitiza kuwa hata kama wanataka kufanya ushirikiano wa kibiashara na Marekani lengo kubwa ni kuhakikisha wakulima kwenye sekta ya maziwa inalindwa ipasavyo.Katibu mkuu mtendaji wa Mamlaka hiyo Margaret Kibogy amesema Kenya hivi sasa inalenga kuuza bidhaa zake za maziwa katika soko la Afrika ambalo limecheleweshwa na janga la corona.

  Wiki iliyopita, wakulima wa bidhaa za mawziwa walipinga hatua ya Marekani ya kutaka kupenyeza bidhaa zake katika soko huru kwenye makubaliano kati yake na Kenya. Aidha wakulima hao walikasirishwa na hatua ya sekta ya bidhaa za maziwa ya Marekani kusukuma makubaliano ya kibiashara ya kutaka kupunguziwa ushuru kwa bidhaa watakazosafirisha kwa soko la Kenya pindi makubaliano hayo yatakapotekelezwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako