• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaitaka Marekani kuweka mazingira bora kwa wawekezaji wa China

    (GMT+08:00) 2020-08-21 19:25:53

    Serikali ya China imeitaka Marekani kuacha kuwakandamiza wafanyabiashara Wa China na badala yake kuboresha mazingira ya kiuchumi na biashara kati ya nchi hizo mbili kwa manufaa ya watu wa pande zote mbili.Msemaji wa wizara ya biashara ya China Gao Feng alisema hayo kufuatia hatua ya Marekani ya kupiga marufuku program ya Til Tok ambayo hutumiwa kwa kuangalia video.

    Gao amesema kwa muda sasa Marekani imekuwa ikitumia kisingizio cha usalama wa taifa kuzizuia kampuni za China kuendeleza uwekezaji wake na shughuli za kibiashara katika nchi hiyo ikiwemo kuziwekea vikwazo vya kibiashara bila kuzingatia sheria. Gao anasema hatua hiyo inahujumu haki na nia njema ya wafanya biashara wa China na pia inavynja kanuni muhimu za soko la uchumi.

    Ameongeza kuwa vikwazo hivyo vya Marekani kwa hakika vitahujumu imani ya wawekezaji nchini humo.

    China imesema inapinga vikwazo vinavyowekewa wawekezaji kwa kutumia kisingizio cha usalama wa taifa na kusisitiza kuwa itaendelea kujitolea katika kulinda haki na nia njema ya wafanyabiashara wa China katika nchi za kigeni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako