• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yaahidi kulinda mradi wa reli ya TAZARA

    (GMT+08:00) 2020-08-21 19:26:43

    Tanzania imeihakikishia Serikali ya China kuwa mradi wa reli ya Tanzania-Zambia (TAZARA) uliojengwa kwa msaada wa China hautokufa kwa kuwa una manufaa makubwa kwa Watanzania.

    Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa kitabu cha kumbukumbu ya Urafika Kati ya China na Afrika, waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Profesa Palamagamba Kabudi amesema serikali ya China imekuwa na uhusiano mzuri na Tanzania kwa muda mrefu. Ameongeza kuwa Tanzania ilipata msaada wa kujenga reli hiyo kutoka kwa China wakati ilikuwa masikini.

    Profesa Kabudi aliongeza kuwa serikali ya China imekuwa ikitoa misaada mingi nchini humo hasa katika sekta za kilimo, jeshi na viwanda.

    Aidha waziri huyo alisema serikali ya Tanzania ilitoa Sh. bilioni 10 kwa ajili ya maboresho ya reli hiyo na kulipa mishahara kwa baadhi ya wafanyakazi wa reli hiyo.

    Kwa upande wake, msaidizi Mkuu wa Meneja Mkuu wa TAZARA, Jofrey Sengo, alisema Sh. bilioni 10 zilizotolewa na serikali kwa ajili ya maboresho ya reli hiyo zimesaidia pia kuongeza morali ya watumishi wao.

    Katika hafla hiyo, Balozi wa China nchini Tanzania Wang Ke, aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kushirikiana na China, akisisitiza kuwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili ni mzuri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako