• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • GOLF: Mashindano ya Golf ya mwisho wa mwezi yafanyika Lugalo

    (GMT+08:00) 2020-08-24 16:23:33
    Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika MAshariki nchini Tanzania Dkt. Damas Ndumbaro ameipongeza klabu ya Golf ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kutokana na umahiri wake katika michezo. Akizungumza wakati wa kuhitimisha mashindano ya mwisho wa mwezi ya Zantel Monthly Mug yaliyofanyika Lugalo jijini Dar es Salaam, Dkt. Ndumbaro amesema uwepo wa Lugalo ndio msingi wa mafanikio ya mchezo wa Golf nchini Tanzania. Naye mwakilishi wa timu ya wazee wa Klabu ya Generals Dkt. Edmund Mndolwa amesema, huu ni wakati wa wadau kuiunga mkono Lugalo ili iwe kiwanda bora nchini Tanzania na Afrika Mashariki katika kutoa wachezaji bora wa Golf.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako