• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: Watanzania zaidi watakiwa kuanzisha viwanda vya kuzalisha mbolea

  (GMT+08:00) 2020-08-24 18:35:26
  Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya, amesema wakati Serikali ya awamu ya tano ikiendelea kuhakikisha wakulima wanaongeza uzalishaji wa mazao ya biashara na chakula, wawekezaji wanahamasishwa kuanzisha viwanda vya mbolea ili nchi ijitosheleze.

  Kusaya aliwataka Watanzania kuanzisha viwanda vya mbolea ambayo inahitajika kwa wingi zaidi wakati huu kilimo kikiwa ni biashara na kinaajiRi asilimia 58 wananchi na kuchangia malighafi za viwandani kwa asilimia 65.

  Alisema mahitaji ya mbolea za viwandani yameongezeka nchini kutokana na hamasa kubwa na wakulima kujitokeza kulima zaidi ikiwa ni mafanikio yaliyopatikana na Wizara ya Kilimo kwa ushirikiano na sekta binafsi.

  Alisema mahitaji ya mbolea kwa mwaka ni tani 664,000 wakati uzalishaji kwenye viwanda umefika tani 30,000 ya mbolea hivyo kuwa na uhitaji mkubwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako