• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Serikali imepoteza zaidi ya ushuru wa shilingi bilioni 70 tangu kuzuka kwa corona

    (GMT+08:00) 2020-08-24 18:35:44
    Serikali ya Kenya imepoteza ushuru wa shilingi bilioni 71.5, pesa za Kenya kwa mieiz mitano iliyopita, tangu kuzuka kwa janga la virusi vya corona. Virusi hivi vimesababisha biashara nyingi kufungwa, huku wengi wakipoteza ajira zao kufuatia masharti makali yaliyowekwa ili kuthibiti msambao wake.

    Ripoti ya hivi punde inaonyesha kwamba halmshauri ya ukusanyaji ushuru nchini Kenya (KRA), yalikusanya shilingi bilioni 575.9 kutoka kwa walipa ushuru, kati ya mwezi Machi na Julai mwaka huu. Mapato haya yalipungua kwa asilimia 11 ikilinganishwa na shilingi bilioni 647.4 zilizokusanywa kwa kipindi sawa na hiki mwaka uliopita.

    Mwezi Juni mwaka huu ulikuwa mmbaya zaidi kwa KRA. Katika mwezi huo, ushuru uliokusanywa ulipungua kwa kiasi cha shilingi bilioni 27.4 kutoka shilingi bilioni 150.9, mwezi huo mwaka jana.

    Sekta nyingi ambazo serikali hutoza ushuru zimesalia kufungwa. Baadhi yazo ni hoteli, shule, maeneo ya burudani na baa. Wamiliki wa biashara hizi wanatarajia kwamba huenda Rais akalegeza kamba wiki hii, na kuruhusu baadhi ya biashara hizi kurejelea huduma zake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako