• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uganda: URA yakusanya ushuru zaidi mwezi Julai

  (GMT+08:00) 2020-08-24 18:36:00
  Mamlaka ya Ukusanyaji Ushuru nchini Uganda URA, yamekusanay ushuru zaidi mwezi Julai mwaka huu, baada ya baadhi ya wananchi na mashirika yaliyokuwa yamesita kulipa ushuru kutokana na makali ya janga la virusi vya corona, kulipa.

  URA ilikusanya ushuru wa shilingi trilioni 1.2 pesa za Uganda mnamo mwezi Julai mwaka huu, kinyume na matarajio yake ya shilingi trilioni 1.02. Hii ina maana kwamba kulikuwa na zaidi ya shilingi bilioni 179 zilizokusanywa.

  Ongezeko hili la ushuru uliokusanywa ni ishara nzuri kwa sekta ya fedha nchini Uganda, inapojiandaa kwa mwaka mpya wa kifedha wa 2020/21. Hii ni baada ya serikali kupata wakati mgumu sana katika nusu ya pili ya mwaka wa kifedha wa 2019/20 kukusanya ushuru kutokana na athari za janga la virusi vya corona kwa sekta mbali mbali za uchumi.

  Ulipaji ushuru ulikuwa umecheleweshwa kutokana na serikali kuweka masharti ya kuzuia watu kusafiri na kutangamana.

  Ili kunusuru biashara nyingi, serikali ilisogesha muda wa kulipa ushuru, ambapo wamiliki wa biashara hizi walitakiwa kulipa ushuru wao baadaye.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako