• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Kampuni ya Kenya Power kutafuta huduma za wakusanyaji madeni

    (GMT+08:00) 2020-08-24 18:36:22
    Kampuni ya umeme ya Kenya Power, inatafuta huduma za wakusanyaji madeni ili kuisaidia kudai deni lake la shilingi bilioni tano, pesa za Kenya kutoka kwa wateja wake ambao hawatumii tena huduma zake.

    Hii ni moja wapo ya njia inayopanga kutumiwa na Kenya Power, katika kuhakikisha kwamba wanawakamata wezi wa nguvu za umeme nchini Kenya wanaotumia umeme bila kulipa na kuinyima kampuni hii mapato yake. Hadi sasa, mapato ya Kenya Power yameshuka kwa kiais kikubwa sana, jamboo ambalo huenda likalemaza huduma.

    Kenya Power inadai wateja wake zaidi ya shilingi bilioni 20, pesa ambazo zinapaswa kulipwa na wateja wanaotumia nguvu za umeme. Hata hivyo, kwa kuna deni lingine la shilingi bilioni tano, ambalo Kenya Power inadai wateja wake na limekuwepo kwa miaka mingi sana.

    Deni la Kenya Power limetokana na wateja waliofutilia mbali akaunti zao kwa kutuma maombi maalum, na wale ambao akaunti zao zilifungwa kutokana na wao kutolipa ada zao kwa muda mrefu. Wadeni wakuu ni wakazi wa Naiorbi na Mombasa. Takriban shilingi bilioni 2 ya deni hilo, ni la wakazi wa jiji la Nairobi, huku wale wa Mombasa wakidaiwa shilingi milioni 845.7.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako