• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Vijana 2,000 kupokea mafunzo ya ubaharia

  (GMT+08:00) 2020-08-26 20:10:24
  Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Kenya Peter Munya amesema vijana 2,000 watapewa mafunzo ya ubaharia ili waweze kufanya kazi kwenye mashua za uvuvi.

  Waziri Munya alisema kuna haja ya sekta hiyo kuwa na wataalam wa uvuvi ambao watafanya kazi baharini kwenye mashua za uvuvi kuimarisha sekta hiyo.

  Alisema sekta ya uvuvi wa baharini ina uwezo wa kuajiri mamia ya vijana.

  Hata hivyo alilalamika akisema idadi kubwa ya vijana hao hawana tajriba ya uvuvi ili kuchukua nafasi zilizoko.

  Bw Munya alisema serikali imeweka mikakati kuimarisha sekta ya uvuvi ili kuleta maendeleo nchini.

  Akiongea alipozuru kituo cha Liwatoni ambacho ni maalum kwa kuimarisha sekta ya uvuvi na kilichogharimu serikali Sh318 milioni kukirekebisha, Bw Munya alisema wizara yake imeanza kuwalinda wavuvi na kuimarisha sekta hiyo ili kufufua uchumi wa taifa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako