• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: Kufunguliwa upwa kwa kiwanda cha pamba kwaongeza ushindani

  (GMT+08:00) 2020-08-26 20:11:06
  Kufufuliwa kwa kiwanda cha uchakataji wa pamba cha Chama Kikuu cha Ushirika Kahama (KACU) kumesababisha kuongeza ushindani wa masomo ya zao hilo kwa wamiliki wa viwanda vya uchakataji wa zao hilo kutoka shilingi 850 kwa kilo hadi 900.

  Zainabu Telack, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, aliyabainisha hayo wakati wa ziara yake ya siku moja ya kukagua uzalishaji wa kiwanda hicho ambacho kwa siku kinachakata pamba mabero 95, kikiwa na wafanyakazi 140, huku 33 kati ya hao wakiwa wafanyakazi wa kudumu.

  Alisema baada ya KACU kufufua kiwanda cha uchakataji pamba kimeongeza ushindani wa soko la pamba kwa wamiliki wa viwanda vya pamba na kununua zao hilo kwa shilingi 900 badala ya shilingi 850 iliyokuwa awali.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako