• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Sekta binafsi yawapa elimu wajasiriamali

  (GMT+08:00) 2020-08-26 20:11:27
  Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) imetoa bure elimu ya biashara kwa kikundi cha wanawake wajasiriamali wenye ulemavu wa mwili wa Temeke (UWAVIUTE) jijini Dar es Salaam, ili kuwarahisishia ufanyaji wa biashara, kutunza mahesabu na kutangaza bidhaa zao kupitia mitandao.

  Akizungumza na waandishi wa habari, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Zachy Mbenna, alisema taasisi hiyo ni chombo cha kupazia sauti na kuweka mikakati ya ustawi wa taasisi binafsi ili iweze kufikia malengo ya kuwaunganisha Watanzania na fursa za ndani na nje ya nchi.

  Alisema TPSF imeguswa na kikundi hicho cha wanawake wajasiriamali walemavu ambao shughuli zao ni kushona nguo za vitenge, barakoa mashuka pamoja na vitamba

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako