• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mauzo ya nje ya Uganda kwenda Rwanda yapungua hadi Shs328m

  (GMT+08:00) 2020-08-27 19:27:46

  Kutokana na mzozo wa mpaka uliopo baina ya Uganda na Rwanda,mauzo ya nje ya Uganda kwenda Rwanda yameshuka hadi Shs328m.

  Hiki ni kiwango kidogo ambacho Uganda imeweza kupata kutokana na mauzo yake nchini Rwanda ambapo mauzo hayo yanajumuisha vyuma,saruji,maziwa,bidhaa za urembo na bidhaa za nyumbani.

  Kulingana na takwimu kutoka Benki Kuu ya Uganda,nchi hiyo imeuza kiwango kidogo cha bidhaa kwenda Rwanda,ambapo awali nchi hiyo ilikuwa soko lake kuu la mauzo ya nje.

  Mwezi Juni,mauzo ya nje yalipungua hadi Shs328m ikilinganishwa na Shs52b ambazo nchi hiyo ilipata kipindi sawa na hicho mwaka jana.

  Haijabainika wazi iwapo kupungua huko kumetokana na vikwazo vya janga la Corona.

  Hata hivyo,mzozo wa mpaka kati ya Uganda na Rwanda haujatatuliwa kwa miaka miwili sasa umeleta tatizo la kibiashara lililosababisha mauzo ya nje ya Uganda kupungua kwa asilimia 81.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako