• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Viwanda vya chuma nchini Tanzania vyapewa onyo

  (GMT+08:00) 2020-08-27 19:28:04
  Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC)nchini Tanzania, limeviagiza viwanda vya kuzalisha nondo na chuma nchini humo kuzingatia sera ya mazingira ya mwaka 1997, inayozuia matumizi ya kuni kwenye viwanda vyao.

  Agizo hilo lilitolewa na kaimu Meneja wa NEMC Kanda ya Kati, Novatus Mushi, ambaye alisema matumizi ya nishati mbadala yanafaa kudumishwa kwenye viwanda vinavyozalisha nondo na chuma nchini humo ambavyo baadhi yao vinaendelea kutumia kuni na kusababisha uharibifu mkubwa wa mazingira.

  Alisema lengo la agizo hilo ni kutunza mazingira, vinginevyo vitachukuliwa hatua za kisheria.

  Mushi alisema walishapiga marufuku matumizi ya kuni kwenye viwanda hivyo ambavyo vina matumizi makubwa ya kuni, hivyo kukata miti mingi kwa ajili ya kuwashia matanuru ya kuyeyushia vyuma viwandani kwao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako