• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TENNIS: Osaka asusia mashindano ya Tennis kufuatia kupigwa risasi kwa Mmarekani mwenye asili ya Afrika

    (GMT+08:00) 2020-08-28 17:12:29

    Mcheza tennis raia wa Japan ambaye pia ni mshindi mara mbili wa mashindano ya Grand Slam Naomi Osaka, amejitoa kwenye robo fainali ya mashindano ya wazi ya tennis duniani yanayofanyika New York, Marekani, ikiwa ni kupinga kitendo cha polisi kumpiga risasi Mmarekani mweusi Jacob Blake ambaye hakuwa na silaha huko Wisconsin. Osaka ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter kuwa, hatarajii kitu kikubwa kutokea kwa kujitoa kwake kwenye mashindano hayo, lakini kama akiweza kuanzisha mjadala katika mchezo huo unaomilikiwa zaidi na wachezaji weupe, anaona hiyo ni hatua katika mwelekeo sahihi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako