• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TPSF yawataka vijana kukumbatia kilimo cha mboga na matunda

    (GMT+08:00) 2020-08-28 18:43:43
    Taasisi ya Sekta binafsi nchini Tanzania (TPSF) imesema mboga na matunda ni bidhaa ambazo zina soko la uhakika ndani na nje ya Tanzania na kuwataka vijana kujikita katika kilimo cha mazao hayo kama njia ya kujiajiri haraka na kuushinda umaskini kwa kiasi kikubwa.

    Akizungumza na wakulima wadogo, Mwenyekiti wa Bodi ya TPSF Angelina Ngalula amesema jukumu kubwa la watanzania ni kuzalisha na kupeleka mizigo mingi nje ya nchi na kuleta fedha ya kigeni nchini humo.

    Alisema moja ya changamoto kubwa nchini ni kilimo cha mazoea ambacho kinatoa mazao yasiyokidhi ubora soko.

    Amewapongeza wakulima wa Mazombe na kuahidi kuwapeleka wataalum kutoka Chama cha Wakulima wa Mboga na Matunda Tanzania (TAHA) ili wawape ujuzi unaotakiwa na kuinua kipato chao.

    Katika siku za hivi karibuni wakulima wengi nchini Tanzania wamekuwa wakiiomba serikali iwaunganishe na taasisi za kifedha kwa ajili ya kupata mikopo. Wakulima wengi wamekuwa wakisema changamoto kubwa waliyonayo ni ukosefu wa mitaji ya kuendeleza kilimo cha mboga.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako