Waziri Mpina, alieleza kufurahishwa na mkakati wa TADB wa kuinua sekta muhimu za uchumi na kuziomba benki nyingine kuunga mkono azma ya serikali ya ujenzi wa uchumi wa viwanda
TADB imekipa kiwanda cha Meat King Distributors fedha kuboresha miundombinu ili kuongeza uzalishaji na kwa kununua ng'ombe, mbuzi, kondoo na nguruwe za wafugaji. Waziri Mpina amesifu juhudi hiyo ya TADB.
Mpina alisema wizara yake itaendelea kuunga mkono wawekazaji katika viwanda ambavyo malighafi zake zinategemea mifugo na kusema wizara yake itahimiza ufugaji wa kisasa utakaomfanya mfugaji anufaike zaidi na mifugo yake.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |