• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wabunge wa Kenya Wataka 'Kazi Mtaani' Isimamishwe

    (GMT+08:00) 2020-08-28 18:44:39
    Wabunge wa Kenya wanataka mradi wa serikali, wa 'Kazi Mtaani' usimamishe wakidai unatumika kama mwanya wa kupora fedha za umma.

    Mradi huo ulizinduliwa mnamo Mei kama njia ya kuhakikisha vijana wanajikimu wakati ambapo virusi vya corona vilianza kuripotiwa nchini na kuathiri mapato yao.

    Wabunge walimweleza Waziri wa Fedha Ukur Yattani kwamba mpango huo hauna maana wakisema serikali inafaa kuweka mikakati mipya ya kuhakikisha Kazi Mitaani inafanikiwa.

    Walidai mradi huo unasababisha mgawanyiko mkubwa miongoni mwa vijana huku wengi wao wakifungiwa nje na baadhi kupendelewa kiasi cha kulipwa mara mbili.

    Waliongeza kuwa serikali inahitaji kuhakikisha kwamba vijana wanalipwa vizuri kutokana na kazi za sulubu wanazozifanya.

    Mwenyekiti wa kamati ya Bajeti bungeni Kanini Kega naye alisema mradi huo hausuluhishi tatizo la ukosefu wa kazi miongoni mwa vijana na unafaa kubadilishwa ili ule wa kudumu ukumbatiwe.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako