• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • TANZANIA : SERIKAKI YAAGIZA VIWANDA VYA MBOLEA KUPUNGUZA GHARAMA

  (GMT+08:00) 2020-08-31 15:50:09

  Serikali imeviagiza viwanda vyote vya mbolea nchini kuzalisha mbolea yenye viwango vya juu vya ubora na kuiuza kwa wakulima kwa gharama nafuu ili uzalishaji wa mazao uwe na tija na uchangie katika ukuaji wa uchumi.

  Katibu mkuu wizaa ya Kilimo Gerald Kusaya, aliyasema haya mwishoni mwa wiki jana alipotembelea kiwanda cha mbolea cha Minjingu mkoani Manyara. Bwana Kusaya alisema aliamua kutembelea mikoa yenye viwanda vya mbolea, ili kuona namna wanavyozalisha, ili kuona namna ya kuondoa upungufu mkubwa wa mbolea ndani ya nchi, hali jnayosababisha wakulima kuinunua kwa bei ya juu.

  Katibu huyo alisema mahitaji ya mbolea nchini ni tani 664,000 kwa mwaka. Aidha, viwanda vyote 12 nchini vinazalisha tani 38,000 pekee ya mbolea kwa mwaka.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako