• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Mashabiki wana usongo wa kujua kama leo Messi ataungana na Barcelona kujifua kwa ajili ya msimu ujao wa 2020-21

    (GMT+08:00) 2020-08-31 16:17:07

    Macho yote ya mashabiki leo yanaelekezwa uwanjani Camp Nou, Uhispania kujua iwapo nyota Lionel Messi atakuwa sehemu ya wanasoka wa Barcelona watakaorejea kambini kujifua kwa minajili ya msimu ujao wa 2020-21. Kwa mujibu wa gazeti la Mundo Deportivo, Messi anatarajiwa kususia mpango huo baada ya wakala na baba yake mzazi kuwasiliana na kocha Pep Guardiola kuhusu uwezekano wa Manchester City kumsajili fowadi na nahodha huyo wa Barcelona na timu ya taifa ya Argentina. Mnamo Agosti 25, Messi, 33, aliwataka Barcelona kumwachilia abanduke ugani Camp Nou ilia sake hifadhi mpya kwingineko muhula huu wa uhamisho. Nyota huyo aliwatumia vinara wa Barcelona barua ya faksi akieleza kwamba angependa kifungu kwenye kandarasi yake kinachompa idhini ya kuagana na miamba hao wa soka ya Uhispania bila ada yoyote kitekelezwe haraka iwezekanavyo. Barcelona wamesisitiza kwamba kifungu hicho kilipitwa na wakati na kwa hivyo anasalia kuwa mchezaji wao hadi mwishoni mwa mwaka wa 2021. Kwa mujibu wa Barcelona, yeyote anayetaka kumsajili Messi kwa sasa atalazimika kuweka mezani kima cha Sh89 bilioni ili kuwashawishi kumwachilia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako