• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Somalia yatoa masharti kwa kenya kabla ya kurejelea biashara ya miraa

  (GMT+08:00) 2020-09-01 20:03:53
  Serikali ya Somalia imeipa Kenya masharti matano kabla ya kuondoa kizuizi cha uagizaji wa miraa.

  Chama cha Wafanyabiashara wa Miraa cha Nyambene (Nyamita) kimesema kuwa mazungumzo ya kumaliza mzozo wa biashara hiyo yamegonga mwamba na Somalia imetoa masharti ambayo lazima yashughulikiwe na Kenya.

  Masharti hayo ni pamoja na; Kenya lazima iichukue Somalia kama mshirika mwenza, kuepuka kuingilia mambo ya ndani ya Somalia, iombe radhi kwa kukiuka amri za anga ya Somalia, iruhusu bidhaa kutoka Somalia ikiwa ni pamoja na samaki, mchele, sukari, asali, nyama na maziwa na Kenya kuacha kulazimisha safari kutoka Somalia kutua kwanza mjini Wajir kwa ukaguzi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako