• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TENISI: Andy Murray aingia kwa kishindo Michuano ya Wazi ya Marekani

    (GMT+08:00) 2020-09-02 16:30:48

    Muingereza Andy Murray alicheza mechi yake ya kwanza ya Grand Slam tangu mwaka 2019 na kushinda dhidi ya Mjapan Yoshihito Nishioka katika mchezo wake wa raundi ya kwanza ya michuano ya wazi ya Marekani. Kwa mara ya mwisho Murray kushiriki michuano ya Grand Slam ilikua ni kwenye michuano ya wazi ya Australia mwaka jana mwezi Januari, alishinda kwa seti tano 4-6 4-6 7-6 (7-5) 7-6 (7-4) 6-4 akitumia saa nne na dakika arobaini na nane. Murray alitumia siku 596 kuuguza majeraha ya nyonga na sasa yeye na Dovak Djokovic ndio nyota wanaopewa nafasi ya kutwaa taji la US Open kutokana na kukosekana kwa Roger Federer aliye majeruhi na Bingwa mtetezi Rafael Nadal ambaye alijiondoa kwa hofu ya Corona. Kwa upande wa wanawake Johanna Conta amefuzu raundi ya pili kwa kumshinda Hearther Watson kwa seti 7-6 (9-7) 6-1.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako