• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Baba mzazi wa Lionel Messi akutana na rais wa Barcelona

    (GMT+08:00) 2020-09-03 18:41:23

    Baba yake Lionel Messi ambaye pia ni wakala wake, Jorge, wamekutana na rais wa Barcelona Josep Maria Bartomeu, aliyesema kwamba klabu hiyo haitafanya mazungumzo ya kumuuza mshambuliaji huyo wa Argentina, 33. Jorge Messi aliwasili katika uwanja wa ndege wa El Prat akitokea Argentina jana Jumatano ili kwenda kuweka mambo sawa kati ya nyota huyo na klabu. Akiwa uwanja wa ndege mzee huyo alisema kuwa hafahamu kitu chochote kile wakati akiulizwa na waandishi wa habari. Mkutano wa kwanza tangu Messi kutoa ombi la kuondoka klabu hiyo ukiishia bila makubaliano huku Barcelona ikisema ofa ya miaka miwili kwa mchezaji huyo bado ipo. Kima cha malipo ili Messi aruhusiwe kuondoka Barcelona huenda kikawa kidogo pengine hata euro milioni 100.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako