• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rwanda-Bei ya mafuta na bidhaa za petroli yaongezeka kwa mara ya kwanza mwaka 2020

  (GMT+08:00) 2020-09-03 19:38:06

  Mamlaka ya udhibiti wa kawi nchini Rwanda (RURA) imetoa bei mpya za mafuta,ambazo zimeanza kutumika leo alhamisi tarehe 3 Septemba.

  Mafuta yaliyopanda bei ni pamoja na petrol na dizeli.

  Hii ni mara ya kwanza bei za bidhaa za petrol imeongezeka tangu kuanza kwa mwaka huu,na haswa tangu mlipuko wa janga la corona ulipoanza.

  Kuanzia Sepetmaba 3,lita moja ya petrol itagharimu Rwf966, kutoka Rwf908 ilhali bei ya dizeli imeongezeka hadi Rwf943 kutoka Rwf883.

  RURA ilitangaza bei hizo mpya katika taarifa iliyoitoa jana jioni.

  Mamlaka hiyo haikutaja sababu za zlizochangia ongezeko hilo,lakini kushuka kwa bei miezi kadhaa iliyopita kumesababisha hali tete katika soko la kimataifa.

  Bei ya mafuta imekuwa ikishuka sana hivi karibuni.Mwezi Mei,bei ya lita moja ya petrol ilipungua kutoka Rwf1,088 mwezi Machi hadi Rwf965. Wakati huohuo bei ya mafuta ya dizeli ilishuka kutoka Rwf1,073 hadi Rwf925.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako