• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania-Serikali yawataka waganga wa tiba asilia na tiba mbadala kuitumia fursa ya Tanzania ya viwanda kwa kuanzisha viwanda vidogo vya kuchakata dawa

    (GMT+08:00) 2020-09-03 19:38:43
    Serikali ya Tanzania imewataka waganga wa tiba asilia na tiba mbadala kuitumia fursa ya Tanzania ya viwanda kwa kuanzisha viwanda vidogo vya kuchakata dawa zitakazouzwa ndani na nje ya nchi, ili kuongeza pato la taifa kupitia sekta hiyo.

    Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Prof. Mabula Mchembe, alisema hayo jana wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya Siku ya Tiba Asilia ya Mwafrika katika viwanja vya Nyerere Square, jijini Dar es Salaam.

    Alisema, waganga wa tiba asili wanatakiwa kuitumia fursa hiyo kwa kuanzisha viwanda vidogo vitakavyokuwa na uwezo wa kuchakata dawa zenye viwango.

    Prof. Mchembe alisema kwa kutumia viwanda vidogo, waganga hao watazalisha dawa nyingi na zenye viwango ili kuziuza ndani na nje ya nchi,na kujikwamua kiuchumi na kuongeza pato la taifa.

    Aliliagiza Baraza la Taifa la Tiba Asili na Tiba Mbadala kuongeza jitihada katika kusajili dawa zinazotengezwa na waganga nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako