• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • USHINDANI WA KENYA KIVINDA WASALIA PALE PALE DUNIANI.

    (GMT+08:00) 2020-09-04 16:43:12
    Kenya imeshindwa kusonga mbele kwenye msimamo wa ushindani wa sekta ya kiviwanda duniani. Kwenye ripoti ya uchunguzi ya hivi punde iliyotolewa na shirika la umoja wa mataifa kuhusu maendeleo ya viwanda, Kenya iko katika nafasi ya 115 kati ya mataifa 152.

    Msimamo huu unaiweka Kenya nyuma ya mataifa ya kama vile Misri inayoshikilia nafasi ya 64 na Afrika Kusini inayoshikilia nafasi ya 52 .

    Hata hivyo, katika ukanda wa Afrika Mashariki, Kenya inaongoza. Tanzania, Uganda na Rwanda ziko nyuma ya Kenya. Tanzania inashikilia nafasi ya 123 kwa ustawi wa viwanda katika orododha ya Umoja wa Mataifa. Uganda inashikilia nafasi ya 128 huku Rwanda ikiwa ya 142.

    Msimamo huu hafifu kwa mataifa ya Afrika Mashariki umechangiwa pakubwa na matumizi ya chini ya teknolojia ya kisasa katika uzalishaji ndani ya viwanda.

    Hata hivyo, Kenya imepigwa jeki na utafiti wa Benki ya Dunia kuhusu mazingira bora ya kufanyia kazi. Ripoti hiyo ya kibiashara ya Benki ya Dunia inasema kwamba Kenya imepanda hadi nafasi ya 56 katika upatikanaji wa mazingira bora ya kufanyia biashara.

    Kwa upande mwengine, wazalishaji wa viwanda nchini Kenya wamelalamika vikali kuhusu gharama ya juu ya uzalishaji wa bidhaa kwenye viwanda hivyo, kutokana na bei ya juu ya nguvu za umeme na mfumo wa ulipaji ushuru usiotabirika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako