Akizungumza wakati wa kukabidhi hundi, mwenyekiti wa bodi ya Airetl Tanzania, Pascal Malata, alisema kiasi hicho cha fedha ni sehemu ya faida iliyopata kampuni.
Malata alisema shilingi bilioni 18.99 zimetolewa kama gawio serikalini kutokana na kuwa na hisa za asilimia 49, Airtel ikibaki kumiliki hisa za asilimia 51 kwenye kampuni. Alisema pia Airtel imetoa shilingi bilioni 14 ukiwa mchango wa kampuni kwa jamii katika maeneo ya kutoa huduma mbalimbali.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |