• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • MTN RWANDA KUTOFANYA MATANGAZO YA KIBIASHARA MWEZI HUU

  (GMT+08:00) 2020-09-04 16:43:56
  MTN Rwanda imetnagaza kwamba haitafanya matangazo ya kibiashara mwezi huu wa tisa, na badala yake, bajeti hiyo kuelekezwa katika mfuko wa fedha wa kukabiliana na virusi vya corona.

  Kwenye taarifa vyake iliyotolewa mapema wiki hii, kampuni hiyo ya mawasiliano inajipa jukumu la kuhamasisha umma umuhimu wa kuvaa maski, ikiwa njia moja ya kukabiliana na virusi vya corona. Kampuni hiyo inazindua kampeni kwa jina Wear It for Me katika mataifa 21 Afrika na mataifa ya Mashariki ya Kati.

  Mwanzoni mwa mwezi Agosti mwaka huu, MTN ilidokeza kwamba itasitisha shughuli zote za kibiashara katika mataifa ya Mashariki ya Kati na kuzingatia Afrika pekee. Mataifa ya Mashariki ya Kati yatakayoathirika ni Syria, Yemen na Afghanistan.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako