• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yalipa ada yote ya mwaka huu kwa Umoja wa Mataifa

    (GMT+08:00) 2020-09-04 20:05:43

    Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying leo amesema, China ikiwa ni nchi ya pili kulipa ada nyingi zaidi kwa Umoja wa Mataifa, imelipa ada yote ya mwaka huu, na kuunga mkono umoja huo kwa kazi zake halisi.

    Amesema, China itaendelea kutekeleza wajibu wake wa kifedha katika Umoja wa Mataifa ikiwa nchi inayoendelea.

    Habari zinasema, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres hivi karibuni aliwaandikia barua nchi wanachama wa umoja huo, na kueleza kuwa Umoja wa Mataifa unakabiliwa na shida kubwa ya kifedha. Amezitaka nchi wanachama hao kulipa ada kwa wakati na kwa ukamilifu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako