• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mabondia Twaha Kidudu na Dullah Mbabe kupanda ulingoni Desemba 26

    (GMT+08:00) 2020-09-07 16:53:09

    Wanamasumbwi wa kulipwa nchini Tanzania Twaha Hassan 'Twaha Kidudu na Abdallah Pazi 'Dullah Mbabe' wanatarajia kupanda ulingoni Desemba 26 mwaka huu kuzichapa katika pambano la usiku wa mabingwa. Pambano hilo limepangwa kufanyika katika Ukumbi wa Club Next Door, mjini Dar es salaam. Kiduku na Dulla Mbabe ambao wametoka kupigana wikiendi iliopita wapanda ulingoni katika pambano kwa kucheza na mabondia kutoka nchini Malawi. Mbali na mabondia hao, mabondia wengine watakaopanda ulingoni kwenye mapambano ya utangulizi ni Mfaume Mfaume atazichapa na Chikondi Makawa wa Malawi. Selemani Kidunda kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania akitarajia kucheza dhidi ya Limbani Masamba, na mwenzake Ismail Isaac 'Gari ya Tano' atapambana Baina Mazora, huku Tonny Rashid atetea mkanda wake dhidi ya Mzimbabwe Tinashe Mwadziwana .

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako