• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kamisha TRA aeleza sababu makusanyo kupanda maradufu

    (GMT+08:00) 2020-09-07 17:21:19

    Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Dk. Edwin Mhede, amesema kwa sasa makusanyo kwa mwezi ni Sh. trilioni 1.5 ambazo ni ongezeko la asilimia 76 ikilinganisha Sh bilioni 850 zilizokuwa zikikusanywa kwa mwezi kabla ya Serikali ya awamu ya tano.

    Alisema hayo mwishoni mwa wiki jana huko Mbeya, wakati wa kikao kazi cha tathmini ya utendaji kazi wa Idara ya Kodi za Ndani.

    Alisema jitihada za Serikali ya awamu ya tano katika ngazi zote imechangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la makusanyo hayo ikiwa ni pamoja na kuzuia mianya ya ukwepaji kodi, kuhamasisha matumizi ya mashine za kielektroniki (EFD) na kudhibiti nidhamu na uadilifu kwa watumishi wa TRA. Alisema TRA imekuwa ikichukua hatua mbalimbali katika kuhakikisha watumishi wake wanafanya kazi kwa uadilifu na uwajibikaji na kwamba katika kuhakikisha suala la maadili linazingatiwa, mamlaka hiyo imeunda idara maalum inayosimamia maadili na uadilifu wa watumishi hao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako