• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Mashirika ya serikali ni miongoni mwa wadeni wakuu wa Kenya Power

  (GMT+08:00) 2020-09-07 17:22:01

  Sasa imebainika wazi kwamba changamoto za kifedha inazopitia kampuni ya Kenya Power kuendesha shughuli zake, huenda zimechangiwa pakubwa na baadhi ya taasisi za serikali. Kulingana na ripoti iliyochapishwa kwenye gazeti la Daily Nation mwishoni mwa wiki jana, taasisi za serikali zinaongoza kwa kutolipa madeni yake ya kutumia za umeme kwa kampuni ya Kenya Power. Kwa mujibu wa gazeti hilo, taasisi za serikali, serikali kuu na zile za kaunti, zinadaiwa takriban shilingi bilioni 4.7. Hii ni kufikia mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu.

  Serikali haijakamilisha malipo yake ya mabilioni ya pesa kwa kampuni ya Kenya Power, katika mradi wa kitaifa wa kusambaza nguvu za umeme mashinani. Deni la serikali limepanda na kufikia shilingi bilioni 11.95, jambo ambalo linaonekana kuwa ni serikali kuu kuumiza mojawapo ya taasisi yake ambayo ni Kenya Power, kiuchumi.

  Mkurugenzi Mkuu wa Kenya Power alinukuliwa akisema kwamba, imekuwa vigumu kwao kudai serikali kuu deni na kulazimika kutafuta msaada wa hazina ya kitaifa. Ni kutokana na hatua hii ya kuhusisha hazina ya kitaifa, ndipo baadhi ya taasisi za serikali zimeanza kulipa madeni yake.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako