• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Forbes Magazine yapiga jeki utalii nchini Kenya.

  (GMT+08:00) 2020-09-07 17:22:19

  Jarida la Forbes limeiweka Kneya kwa orodha ya mataifa tisa ambayo yako tayari kwa ufunguzi wa utalii na safari za kibiashara. Habari hizi zimepokelewa vyema sana na wadau katika sekta ya Utalii nchini Kenya.

  Shirikisho la Utalii Kenya (KTF), mwavuli wa utalii, limesema kwamba hatua hii ya kutambuliwa na jarida la Forbes ni ishara tosha kwamba Kenya imetimiza masharti yanayohitajika kimataifa, kuhus afya na kwa sasa ni salama kwa watalii wa nje na ndani ya taifa hilo. Aidha, hii pia ni ishara kwamba harakati na mikakati ya Kenya katika mapambano na janga la COVID-19, zinazaa matunda.

  Wamiliki wa hoteli za kitalii pia wamefurahia sana hatua hii na huenda wakaaza kupokea watalii wa kigeni . Sekta hii ni mojawapo ya setka zilizoathirika vibaya zaidi na janga la corona nchini Kenya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako