• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchumi wa Uganda unarejea kwa kasi licha ya makali ya virsusi vya corona.

    (GMT+08:00) 2020-09-07 17:22:36

    Uchumi wa Uganda umeanza kupanda kwa asilimia 4.9 ya pato la ndani la taifa yaani GDP, baada ya kushuka chini hadio asilimia 2.9 wakati taifa liliweka masharti makali ya kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya corona.

    Haya ni kwa mujibu wa waziri wa Biashara, Viwanda na Mashirika Amelia Kyambadde, ambaye amsema kwamba uchumi wa Ugandsa umeanza kukua kwa kasi tena baada ya makali ya covid-19.

    Hata hivyo, waziri alielezea wasiwasi wake kwa sekta ya mali isiyohamishika, ambayo huenda ikachukuwa muda mrefu zaidi kujikwamua. Hii ni kwa sababu, wafanyibiashara wengi wamesusia kukodi vyumba na kuanza kuuza bidhaa na huduma zao mitandaoni

    Ili kusaidia taifa kujikwambua kiuchumi, bi Kyambadde amewahimiza Waganda kununua bidhaa zinazozalishwa nchini mwao kwa wingi, ili kuinua kampuni za nyumbani. Hata hivyo, kampuni nazo zimetakiwa kuzalsiha bidhaa zenye ubora wa juu na bei nafuu ili kuwavutia wateja wengi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako