• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Biashara kati ya China na nchi za nje yaendelea kuwa na ongezeko tulivu huku hatua za kuunga mkono zikiendelea

    (GMT+08:00) 2020-09-07 18:19:53

    China imeendelea kushuhudia kufufuka kwa biashara na nje wakati hatua za serikali kuunga mkono makampuni kwenye sekta ya biashara na nje zikiendelea.

    Takwimu kutoka Idara kuu ya usimamizi wa forodha ya China (GAC) zinaonesha kuwa thamani ya biashara na nje katika mwezi Agosti iliongezeka na kufikia dola za kimarekani bilioni 421.14, thamani ya mauzo ya nje ikiongezeka kwa asilimia 11.6 na thamani ya bidhaa zilizoagizwa ikipungua kwa asilimia 0.5.

    Katika kipindi kati ya Januari hadi Agosti nchi za Asia Kusini Mashariki zimeendelea kuwa mshirika mkuu wa biashara kukiwa na ongezeko la asilimia 7, biashara na Marekani imepungua kwa asilimia 0.4, na uagizaji wa bidhaa kutoka Marekani umeongezeka kwa asilimia 0.2.

    China imekuwa ikichukua hatua mbalimbali za kuhimiza biashara na nchi za nje, na takwimu zinaonyesha kuwa kumekuwa na msamaha wa kodi wenye thamani ya Yuan bilioni 812.8 kwa bidhaa zinazouzwa nje ya nchi katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, ili kupunguza madhara ya COVID-19 kwenye biashara na nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako