• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Janga la COVID-19 huenda kuwafanya watu milioni 100 waangukie kwenye ufakara

    (GMT+08:00) 2020-09-07 18:50:38

    Naibu mwakilishi wa Shirika la mpango wa chakula duniani (WFP) nchini China Bw. Maha Ahmed, amesema kutokana na athari za janga la COVID-19, inakadiriwa kuwa watu milioni 70 hadi milioni 100 wataangukia katika umaskini uliokithiri mwaka huu. Hivi sasa shirika hilo linafanya juhudi kuhamasisha raslimali ili kukidhi mahitaji ya chakula kwa watu zaidi ya milioni 100.

    Mkutano wa 23 wa biashara na uwekezaji kwenye sekta ya uchakataji wa mazao ya kilimo wa China ulifunguliwa huko Zhumadian mkoani Henan, China. Bw. Maha alipotoa pongezi katika ufunguzi wa mkutano huo, akisema kuwa shirika la WFP linatakiwa kutoa mwitikio mkubwa zaidi wa kibinadamu katika historia, ili kutatua tatizo la njaa linalozidi kukithiri duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako