• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China haiweki vizuizi dhidi ya wanahabari wa Marekani

    (GMT+08:00) 2020-09-07 20:02:08

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Lijian, amesema China inashughulikia ombi la kurefusha viza la wanahabari wa Marekani nchini China, na kabla ya hapo wanahabari hao wanaweza kuendelea na shughuli zao nchini China.

    Kauli hiyo imekuja baada ya wizara ya mambo ya nje ya Marekani kudai kuwa China imekataa kurefusha viza za wanahabari wa Marekani, ili kujibu kitendo cha Marekani dhidi ya wanahabari wa China.

    Bw. Zhao amesema tangu mwaka 2018, Marekani imeweka vizuizi mbalimbali dhidi ya wanahabari wa China nchini humo, ikiwemo kukataa kuwapa viza, na kupunguza muda wa viza zao kuwa chini ya siku 90, kuyaorodhesha mashirika ya habari ya China kama wawakilishi wa serikali, na hata kuwafukuza wanahabari wa China.

    Hata hivyo Bw. Zhao amesema China inapenda kutatua suala la wanahabari na Marekani kwa kufuata kanuni ya usawa na kuheshimiana, na hadi sasa haijachukua hatua ya kulipiza kisasi, lakini kama Marekani haitasahihisha makosa yake, China italazimika kulinda haki yake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako