• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yawatunukia watu hodari waliotoa mchango mkubwa katika mapambano dhidi ya COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-09-08 10:50:13

    Leo tarehe 8 China imewatunukia watu waliotoa mchango mkubwa katika mapambano dhidi ya janga la virusi vya Corona. Rais Xi Jinping aliwatunukia nishani na heshima ya kitaifa.

    Nishani ya kitaifa na heshima ya kitaifa ni heshima kubwa zaidi za kitaifa nchini China. Msomi wa Chuo cha Uhandisi cha China, na mtaalamu mashuhuri wa magonjwa ya upumuaji Bw. Zhong Nanshan, ambaye alitambua hali ya maambukizi ya virusi vya Corona kati ya binadamu, na kuongoza maandalizi ya mipango ya matibabu ya ugonjwa huo, alipewa "Nishani ya kitaifa" kwa kutoa mchango mkubwa katika mapambano dhidi ya janga hilo. Wengine watatu waliopewa heshima ya kitaifa ya "mashujaa wa taifa" ni pamoja na wasomi wa Chuo cha Uhandisi cha China Bw. Zhang Boli na Bibi Chen Wei, ambao walitoa mchango mkubwa katika matibabu ya virusi vya Corona na utafiti na uendelezaji wa chanjo ya virusi hivyo, pamoja na mkurugenzi wa Hospitali ya Jinyintan ya Wuhan Bw. Zhang Dingyu ambaye amekuwa mstari wa mbele akishikilia kupambana na virusi vya Corona huku akisumbuliwa na ugonjwa wa kufa kwa neva (Amyotrophic lateral sclerosis ALS).

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako