• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mechi za Nations League zinaendelea tena leo barani Ulaya

    (GMT+08:00) 2020-09-08 16:53:55

    Jana mechi za Nations League ziliendelea tena, na kama niliuvyokufahamisha kwenye kipindi cha michezo cha jana kulikuwa na mechi ya kukata na shoka kati ya Italia na Uholanzi, Italia iliibuka na ushindi wa goli moja kwa bila katika mechi iliyiotarajiwa na wengi kuwa Uholanzi itaibuka kidedea. Timu ya Jamhuri ya Czech ikichezesha timu B, imefungwa mawili kwa moja na timu ya Scotland katika mechi iliyochezwa nyumbani. Waczech walilazmika kuchezesha timu B baada ya mchezaji mmoja wa timu A kukutwa na virusi vya Corona na timu yotwe kuwekwa kwenye karantini ya wiki mbiliā€¦.Mechi zinaendelea tena leo huku kukiwa na mechi tisa. England iko ugenini kukumbana na Denmark wakijaribu bahati yao baada ya ushindi wa bahati dhidi ya Iceland, Sweden baada ya kuchapwa na Ufaransa goli moja kwa bila leo inajaribu bahati yake nyumbani dhidi ya Ureno walioanza kwa ushindi wa magoli manne.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako