• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kocha wa Uingereza asema atasimamia nidhamu, na awaadhibu wachezaji wawili walioleta wasichana vyumbani mwao.

    (GMT+08:00) 2020-09-08 16:54:51

    Kocha wa Uingereza Gareth Southgate amesema atawalinda Mason Greenwood na Phil Foden licha ya kuwatimua wachezaji hao na kuwarudisha nyumbani baada ya kuvuruga maandalizi ya England kwa mchezo wa Jumanne usiku dhidi ya Denmark, kwa kuwaalika wasichana wawili kwenye vyumba vyao hotelini mjini Reykjavik, na kukiuka kanuni za umbali wa kijamii dhidi ya virusi vya Corona. Ingawa Southgate amekiri kwamba Greenwood mwenye miaka 18, na Foden mwenye 20, walikuwa na hatia ya tabia ya "utoto", kocha huyo amesema hapendi kuona wachezaji hao wakikosolewa vikali na wanahabari kutokana na kuwa bado wana umri mdogo. Ufuatiliaji wa wanahabari unatarajiwa kuwa mkali, wakati tayari wamelazimishwa kukosa safari ya England kwenda Denmark, na kila mmoja ametozwa faini Krona 250,000 za Iceland (Pauni 1,300) na polisi, kabla ya kupandishwa ndege na kurudi Manchester. Waliofichua siri hiyo ni kina dada hao ambao waliweka picha kwenye kurasa zao za Snapchat wakiwa na kina kaka hao, na kunaswa na gazeti la DV la ICELAND.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako