• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania WIZARA ya Kilimo kupunguza kiwango cha riba ya mkopo inayohusiana na kilimo hadi chini ya asilimia 10

  (GMT+08:00) 2020-09-08 19:35:47

  WIZARA ya Kilimo inalenga kupunguza kiwango cha riba ya mkopo inayohusiana na kilimo hadi chini ya asilimia 10 ili kukuza sekta hiyo na kuinua ustawi wa watu.

  Wizara imesema mafanikio makubwa yamepatikana baada ya kiwango cha wastani kushuka kutoka asilimia 22 hadi asilimia 13 ya sasa na lengo lilikuwa kuona wakulima wakikopeshwa riba nafuu.

  Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema serikali inaendelea kuweka mazingira mazuri kwa watoa huduma za kilimo kuwawezesha kufanya biashara zao katika mazingira bora.

  Aidha amesema wakulima katika Mkoa wa Tabora wanapaswa kujiandikisha na Mpango wa Action Africa ili kupata mbolea ya bure.

  Lakini, aliwaonya wasitumie vibaya msaada huo, kwani hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wale wanaokiuka kanuni.

  Yara Tanzania ilizindua Action Africa ili kusaidia wakulima wadogo kwa kutoa mbolea za bure. Mpango huo unalenga kufikia zaidi ya wakulima 83,000 - haswa wale wanaolima mpunga na mahindi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako