• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wanasiasa na wasomi wa Kenya wapongeza mafanikio ya China katika kupambana na janga la virusi vya Corona

  (GMT+08:00) 2020-09-09 18:14:28

  Mkutano wa kutunuku tuzo kwa watu waliotoa michango mikubwa kwenye mapambano dhidi ya virusi vya Corona nchini China ulifanyika jana mjini Beijing. Wanasiasa na wasomi wa Kenya wamepongeza mafanikio ya China katika kupambana na janga la virusi hivyo. Wanaona China imetekeleza ipasavyo wajibu wake kwenye mapambano ya kimataifa dhidi ya janga hilo, na kubeba majukumu yake kama nchi kubwa inayowajibika.

  Akihutubia katika Mkutano wa kutunuku tuzo kwa watu waliotoa michango mikubwa kwenye mapambano dhidi ya virusi vya Corona nchini China, Rais Xi Jinping amesema tangu mlipuko wa virusi vya Corona utokee, China imeshirikiana kwa karibu na nchi mbalimbali duniani katika kukabiliana na changamoto kwa pamoja, na kuchangia busara na nguvu kwenye mapambano ya kimataifa dhidi ya virusi hivyo.

  Virusi vya Corona bado vinaendelea kusambaa barani Afrika. Mpaka sasa serikali ya China imetoa misaada mingi ya vifaa tiba kwa Umoja wa Afrika na nchi za Afrika, na misaada hiyo imesafirishwa katika nchi 20 za Afrika zisizo na bandari chini ya ushirikiano kati ya China na Afrika. Mbali na hayo, China pia imetuma timu za wataalamu wa matibabu kwenye nchi 13 za Afrika kutokana na mwaliko wa nchi hizo.

  Mkurugenzi wa masuala ya kisiasa wa muungano tawala nchini Kenya, Jubilee, Bw. Kadara Swaleh amesema, China imebeba wajibu na majukumu yake kama nchi kubwa inayowajibika katika kukabiliana na janga hilo.

  "China imetoa teknolojia, ufundi, uzoefu, vifaa tiba na misaada mingine mingi kwa nchi na sehemu mbalimbali duniani. Tunaishikuru sana China, ilitoa uzoefu wake wa kupambana na janga la virusi vya Corona, na kutoa vifaa tiba kwa Afrika na sehemu nyingine duniani, misaada ambayo haitasahaulika kamwe. Methali ya Kiswahili inasema, hata kwenye janga kuna mwanga. Tunachokiona ni kwamba katika kukabiliana na msukosuko huu wa kimataifa, China imehimiza mshikamano wa dunia, imeisaidia dunia, na haijawahi kuleta mgawanyo katika dunia yetu."

  Akizungumzia mafanikio yaliyopatikana nchini China katika kudhibiti janga hilo, mkurugenzi wa vitivo katika Chuo kikuu cha Aga Khan nchini Kenya Dkt. Alex Awiti, amesema serikali ya China ilifanya maamuzi sahihi na ya haraka katika kupambana na janga la virusi vya Corona.

  "Moja ya sababu kwa China kuweza kushinda janga la virusi vya Corona, ni kwamba China ilitoa mwitikio wa makini na wa haraka kwa janga hilo. China ilitambua kwa haraka kuwa hili ni tishio dhidi ya afya ya umma na uchumi wa China, na mara moja ilitekeleza hatua madhubuti za kuzuia kuenea kwa virusi na kufunga miji, hatua ambayo imeonesha ufanisi mkubwa. Uchumi wa China kwa sasa umeanza kufufuka."

  Kwenye hotuba yake, Rais Xi Jinping amesema China imesaidia kivitendo kuokoa maisha ya mamia ya maelfu ya watu kote duniani, na pia imeonesha kivitendo matumaini yake ya dhati ya kusukuma mbele ujenzi wa Jumuiya ya Binadamu yenye Hatma ya Pamoja.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako