• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe kufunguliwa

    (GMT+08:00) 2020-09-09 18:25:26

    Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe nchini Uganda unatarajiwa kufunguliwa tena Oktoba 1, 2020, kwa safari za ndege za kimataifa, baada ya kufungwa kwa miezi 5.

    Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Uganda (UCAA) imeruhusu zaidi ya mashika ya ndege 15 kutua kwenye uwanja huo.

    Miongoni mwa mashirika ya ndege yanatarajiwa kuanza tena safari za ndege nchini Uganda ni pamoja na , Kenya Airways, Qatar Airways, Air Tanzania, Shirika la ndege la Ethiopia, FlyDubai, RwandAir na KLM.

    UCAA inasema itaendelea kufungulia mashirika mengine taratibu.

    Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Entebbe ulifungwa tangu Machi wakati maambukizi ya corona yaliporipotiwa nchini humo.

    Ufungaji huo umeathiri hasa sekta ya utalii ambayo hutegemea sekta ya usafiri wa anga.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako